Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PURA yatanua misuli mradi gesi asilia

Gesiii PURA yaeleza ilivyojipanga kusimamia mradi wa LNG

Wed, 18 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA) imeeleza kuwa imejipanga kikamilifu kusimamia mradi wa kubadili gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) ili kuhakikisha mradi huo unaleta tija na kuchangia maendeleo ya uchumi nchini.

Hayo yamesemwa na Mjiolojia Fortunatus Kidayi alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa waLindi, Mhe. Zainab R. Telack aliyetembelea banda la PURA katika Maonesho ya Tano ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea mkoani Morogoro.

Alifananua kuwa miongoni mwa majukumu ya PURA kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 nikusimamia mradi wa LNG. Mradi huu unalenga kuvuna gesi asilia iliyogunduliwa kwenye kina kirefu cha bahari nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani na kiasi kingine kuuzwa nje ya nchi.

“Mradi huu ni wa thamani ya Dola za Marekani bilioni30 na unatarajiwa kutekelezwa eneo la Likong’o mkoani Lindi na PURA imeendelea kujiimarisha kiutendaji ikiwemo kuendelea kuwajengea watumishi wake uwezo katika eneo la LNG” alieleza Bw. Kidayi.

Aliongeza kuwa PURA imejipanga kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kushiriki katika mradiwa LNG kupitia ajira na utoaji wa huduma na bidhaa katika kipindi chote cha utekelezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live