Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PURA yashawishi uwekezaji mafuta, gesi asilia

9f762e9de4a857a5f26660a96af59d1e PURA yashawishi uwekezaji mafuta, gesi asilia

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Sangweni amesema Tanzania ina fursa nyingi za gesi na kutaka kampuni za ndani na nje kuwekeza katika utafutaji na uchimbaji ili wananchi wanufaike na fursa za ajira kwenye maeneo husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Arusha katika maonesho ya nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi yanayoendelea katika viwanja vya Shekhe Amri Abeid alisema maeneo yanapofanyika tafiti za mafuta na gesi hali ya uchumi kwa watanzania wazawa inaimarika sababu kutakuwa na huduma muhimu za malazi na vyakula.

Alisema Pura ina malengo ya kurasimisha uwekezaji katika mkondo wa juu wa petroli na kuhakikisha mgao wa serikali unaongezeka ikiwemo wazawa katika manunuzi ya bidhaa na huduma katika tasnia ya petroli.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ushiriki wa Wazawa kutoka Pura, Charles Nyangi alitoa rai kwa watanzania kutumia fursa zilizopo kwenye tasnia ya utafiti na uchimbaji wa gesi asili katika kuuza bidhaa na kutoa huduma bora na kuwapiku washindani wao wa nje ya nchi ili kujiongezea tija kiuchumi.

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki maonesho hayo akiwemo Joseph John aliiomba Pura kujitangaza zaidi kwa kutumia vyombo vya habari ili wananchi waweze kutambua fursa za uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na kuchangamkia ajira.

Chanzo: habarileo.co.tz