Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PURA yaibuka kinara maonesho ya bidhaa Zanzibar

21c75372edcc35613e415a2eb650bc55.PNG PURA yaibuka kinara maonesho ya bidhaa Zanzibar

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeibuka kinara katika Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda yaliyomalizika katika viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda visiwani Zanzibar, Omar Said Shaban ameitunukia PURA cheti hicho Alhamisi (Desemba 9, 2021) wakati akihitimisha maonesho hayo yaliyowaleta pamoja jumla ya wadau 113 zikiwemo taasisi za serikali, kampuni binafsi, viwanda vidogo vidogo na wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Mamlaka, Mjiolojia wa PURA Ebeneza Mollel ameeleza kuwa cheti hicho ni matokeo ya juhudi za PURA katika kutimiza jukumu lake la kuuhabarisha umma kuhusu shughuli za mkondo wa juu wa petroli kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo maonesho ya biashara.

“Cheti hiki ni motisha kwetu kuendelea kutoa uelewa kwa Watanzania kuhusu PURA, shughuli inazozifanya na hususani katika kuongeza ushiriki wa wazawa katika shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini,” ameeleza.

Mollel ameongeza PURA imejipanga kuendelea kuwapa taarifa wananchi kuhusu fursa mbalimbali zinazotokana na utekelezaji wa miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia sambamba na kuwajengea uwezo wa kuzitumia fursa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live