Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PURA watakiwa kuongeza juhudi kuinua sekta ya gesi, mafuta

PURAAA PURA watakiwa kuongeza juhudi kuinua sekta ya gesi, mafuta

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu ili kuiletea tija sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka hiyo Mhandisi Charles Sangweni wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

“Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha shughuli za mkondo wa juu wa petroli zinaleta chachu ya maendeleo kwenye mnyororo mzima wa mafuta na gesi asili nchini, na utendaji wetu kama wafanyakazi ndio utafanikisha hili,” alieleza.

Mhandishi Sangweni aliongeza kuwa ni vyema wafanyakazi wote wakajituma katika kutimiza majukumu yao ya kila siku huku wakiongeza ubunifu ili kuongezea thamani katika kile wanachozalisha.

Katika kikao hicho, wajumbe wa Baraza hilo walipata fursa ya kupitia na kujadili taarifa ya mapendekezo ya kuhamisha fedha kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 kutoka idara na vitengo vya taasisi.

Aidha, baraza limejadili taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2022/23, hoja za wafanyakazi na masuala mengineyo yahusuyo utendaji kazi na hali bora kwa wafanyakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live