Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSSSF kutoa ajira 3,000 kwa watanzania

Ajira Mpyaaaaa PSSSF kutoa ajira 3,000 kwa watanzania

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

Uwekezaji wa ubia uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), katika viwanda vinne nchini vinatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 3,000 na zisizo rasmi kwa maelfu ya Watanzania .

Maneja Mipango na Uwekezaji wa Mfuko huo, Herman Gudluck amesema hayo Machi 31, 2023 wakati akiwasilisha mada kuhusu masuala ya uwekezaji kwa wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walioshiriki mkutano wa 12 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Mjini Morogoro.

Gudluck amesema PSSSF imeingia ubia katika ujenzi wa kiwanda cha Chai kilichopo Mponde mkoani Tanga na Kiwanda cha kuchakata tagawizi cha Mamba Myamba kilichopo wilaya ya Same , mkoani Kilimanjaro .

Vingine ni Kiwanda cha bidhaa za Ngozi kilichopo mkoani Kilimanjaro pamoja na Kiwanda cha machinjio ya kisasa ya Nguru Hills kilichopo wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

Amesema viwanda hivyo vyote vitakapokamilika vitagharimu kiasi cha Sh bilioni 164 sawa na asilimia mbili ya mapato ya Mfuko huo na kwamba uwekezaji huo ambao umefanyika kwa ubia bila kuingilia sera zinazoongoza mfuko huo.

Gudluck amesema kiwanda cha tangawizi , Mfuko umeingia ubi ana wakulima wa eeno hilo na kununua mashine mpya kwa uwekezaji wa Sh bilioni nane na hadi sasa kiwanda kimekamilika na kuanza kufanya kazi ya uzalishaji.

Wakati kiwanda cha Chai Mponde ambacho wameingia ubia na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ( WCF), na kwa sasa kipo katika hatua ya mwisho kukamilika , na kwa kiwanda cha bidhaa za Ngozi nacho kinatarajiwa kukamilika mwaka huu (2023).

Gudluck amesema , Kiwanda cha machinjio ya kisasa ya Nguru Hills , Mfuko huo umewekeza kiasi cha Sh bilioni 8.3 na kwa sasa kimeanza kazi ya kuchinja na kuchakata nyama ambazo inasafirishwa kwenda nje ya nchi na nyingine ndani ya nchi.

Chanzo: Habarileo