Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PPP ikusaidia miradi muhimu iliyo nje ya bajeti kuu

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtaalamu wa ubia kutoka Benki ya Dunia, Craig Sugden amesema ubia baina ya Serikali na sekta binafasi (PPP) utasaidia maendeleo ya uchumi wa taifa na upatikanaji wa huduma mhimu.

Sugden amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wadau wa maendeleo ulioandaliwa na Benki ya Dunia, Tamisemi na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ili kupata maoni ya kuandaa rasimu ya mwongozi utakaotumika katika miradi ya PPP.

"Kupitia PPP utekelezaji wa miradi mingi ya kijamii ambayo ni muhimu itaacha kutegemea bajeti kuu hivyo uchumi wa Watanzania utastawi kwakuwa maendelo ya uchumi yanategemea uwepo wa miundombinu thabiti na wakati mwingine kutokana na ufinyu wa bajeti imekuwa haitekelezwi," amesema.

Amesema PPP huchukua jukumu la kutekeleza mambo ambayo bajeti imeshindwa kuyatekeleza hivyo kupitia mpango huo kuna matarajio ya kukua kwa sekta ya kilimo, biashara, huduma za afya, elimu na ujenzi wa miundombinu.

Ofisa kutoka PPRA ambaye alikuwapo katika mkutano huo, Gilbert Kamnde amesema kupitia PPP sekta binafsi inaisaidia Serikali kuleta maendeleo hususan kuhakikisha uwapo wa huduma bora za kijamii.

"Utaratibu wa kutangaza tenda za namna hiyo ni wa wazi, sekta binafsi inaweza kuiona fursa au taasisi ya umma ndiyo ikawa imeona fursa, kwa pamoja watashirikiana , hata hivyo miradi ya namna hii uwekezaji wake ni wa muda mrefu," amesema.

Mkuu wa kitengo cha ubia wa Tamisemi, Hemed Mpili amesema tayari miradi ya ubia inafanyika katika halmashauri za majaribio 10 na mara baada ya kukamilika kwa mwongozo huo na kupata mrejesho wa kilichofanyika katika halmashauri hizo wanatarajia kuhamia katika halmashauri nyingine.

"Mwongozo huu utazisaidia halmashauri katika mchakato wa kuingia ubia kwa urahisi kwakuwa ni gharama kubwa kuandaa mwongozo wa kila mradi kuliko kubadilisha mwongozo mkuu kulingana na mazingira ya mradi," amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz