Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PIC yataka sheria ya uwekezaji iharakishwe

Uchumi Kupanda PIC yataka sheria ya uwekezaji iharakishwe

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Augustino Vuma ameiomba Serikali kuharakisha sheria mpya ya usimamizi wa mashirika na taasisi za umma, akisema sheria hiyo ndio muarobaini wa kutofanya vizuri kwa taasisi nyingi za umma.

Vuma ametoa kauli hiyo Jijini Arusha mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliposimama na kuzungumza na Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa taasisi na mashirika ya umma wanaokutana kwenye kikao kazi.

Ametaja sababu za mashirika na taasisi za umma kushindwa kufanya vizuri kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji, uwezo mdogo wa viongozi wanaosimamia taasisi hizo, kutowajibika kwa watendaji na udhaifu kwenye mifumo ya uendeshaji wa taasisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live