Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onyo la TCRA kwa wanaotuma mizigo bila leseni

B01cc6dab7603fcf5c5be62246cd5db8 TCRA yawapa onyo wanaoendesha shughuli za utumaji mizigo bila leseni

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, imesema kuwa itachukua hatua za kisheria kwa Makampuni na watu wote wanaendesha shughuli za usafirishaji wa mizigo maarufu kama "delivery" kwa njia ya Posta bila kupata vibali kutoka katika mamlaka hiyo.

Mamlaka hii imewataka wanaoendesha shughuli hizi kuhakikisha wanapata vibali maalumu vinavyotolewa na mamlaka hiyo kabla ya tarehe 31 Oktoba .

"Kwa watakao kaidi agizo hili, wajue kuwa TCRA itawachukulia hatua kaliza kisheria" imesema taarifa ya Mamlaka hiyo.

TCRA ni Mamlaka ya kiserikali iliyoanzishwa chini ya sheria namba 12 ya mwaka 2003, ikiwa na majukumu ya kusimamia sekta ya mawasiliano ya kieletroniki nchini pamoja na huduma za Posta kwa maana ya utumaji wa mizigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live