Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Omba karatasi hii kabla hujalinunua

Gari Msgd Omba karatasi hii kabla hujalinunua

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna anayebisha kwamba kitendo cha kukutana na namba E zikiwa nyingi mtaani kinatosha kutupa ishara kwamba idadi ya magari yanayonunuliwa na kuingizwa Tanzania inazidi kuongezeka maradufu siku hadi siku na wengi wetu tunafahamu kwamba Japan ndiko magari 'used' yanakonunuliwa kwa wingi kwenye minada.

Kwa kuwa idadi kubwa ya magari yanayonunuliwa na Watanzania ni yale yaliyokwisha tumika (used), haya ni mambo matano ambayo tunatakiwa tuyazingatie sana kwenye karatasi hii maalum ya ukaguzi (auction sheet) kabla ya kununua gari iwe unalinunulia hapahapa Tanzania au umeliagiza Japan ambapo karatasi hii itakusaidia kufahamu umenunua gari likiwa katika hali gani.

1. Jambo la kwanza ni kwamba karatasi hii (auction sheet) ina madaraja au auction grade kuanzia 0 hadi 5 zikiwa ni alama zinazokuonesha gari hilo liko vizuri kiasi gani ambapo 5 ndio alama ya juu zaidi ya ubora.

2. Kitu cha pili karatasi hii pia inaonesha grade au madaraja ya ukaguzi kuonesha hali ya ndani ya gari na hali ya nje ya gari hivyo kukupa mwanga kama utatakiwa kupita kwa Fundi rangi au Fundi wa interior.

3. Jambo la tatu ni ukaguzi wa mileage unaoonesha gari limetembea kilometa ngapi, hiki ni kipengele kingine muhimu sana unapaswa kukizingatia ili kuepuka baadhi ya Wafanyabiashara wasio waaminifu ambao huzichezea kilometa kwa kuzishusha ili kulifanya gari lionekane jipya zaidi na kumtaka Mteja alipe pesa nyingi zaidi.

4. Kipengele cha nne kinaonesha chassis number, ukubwa wa injini na kama iliwahi kubadilishwa rangi ya gari pamoja na maelezo maalum kutoka kwa Muuzaji kufafanua kama aliwahi kufanya modifications au mambo mengine.

5. kipengele cha tano ni Repair History, maelezo yanayoonesha kama gari limewahi kurekebishwa popote au kufanyiwa ukarabati bila kusahau kipengele cha Diagram, mchoro wa gari ukiwa na alama zinazoonesha sehemu zilizoharibiwa au zilizowahi kukarabatiwa ili upate mwanga.

Swali kwako uliyewahi kununua gari 'used', Je ulipewa hii karatasi na kuisoma kabla ya kulinunua ndinga lako? YES au NO?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live