Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

OPEC kupunguza uzalishaji mafuta ili kuongeza bei

Opec Mafuta OPEC kupunguza uzalishaji mafuta ili kuongeza bei

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la nchi 23 zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani, OPEC ikiwemo Russia pamoja na washirika wengine, limekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta.

Katika mkutano uliyofanyika jana mjini Vienna, OPEC imesema inapunguza uzalishaji wa mapipa milioni mbili kwa siku.

Gavana wa Iran katika kundi la OPEC, Amir Hossein Zamaninia amesema wamekubaliana kupunguza uzalishaji huo kuanzia mwezi Novemba, hatua ambayo inaweza kuongeza bei ya mafuta ghafi.

Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia, Abdulaziz bin Salman amesema OPEC inakusudia kuleta utulivu na uthabiti. Bei ya mafuta ilishuka hadi dola 90 kwa pipa, baada ya kupanda hadi dola 140 kwa pipa mwanzoni mwa vita ya Urusi nchini Ukraine.

Mwezi Julai, Rais wa Marekani Joe Biden aliitolea wito Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wa mafuta. Baadae OPEC ilikubali kuongeza uzalishaji huo, Lakini jana kupitia kikao cha Vienna wamekubaliana kupunguza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live