Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuzi za Mkonge suluhu ya wajasiriamali Zanzibar

Mkonge Katani Nyuzi za Mkonge suluhu ya wajasiriamali Zanzibar

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa Wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Ushirikiano uliopo baina ya Wajasiriamali Zanzibar na Bodi ya Mkonge Nchini utaleta mapinduzi makubwa kwa upande wa Zanzibar katika kuhakikisha Wajasiriamali wadogo wanaozalisha kamba za Usumba wanaachana na matumizi hayo na kuanza kutumia Malighafi zitokanazo na nyuzi za Mkonge.

Mahmoud ameyasema hayo katika Afisi yake Kusini Unguja ambapo amesema Changamoto ya Wajasiriamali imepata suluhu baada ya kupata Malighafi kutoka Tanzania Bara kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao

Amesema Ziara ya Bodi ya Mkonge Tanzania kwenda Visiwani Zanzibar imeweza kuimarisha mashirikiano mazuri baina ya Bodi na Chuo cha Mafunzo Zanzibar ambapo kutakuwa na Ushirikiano wa Moja kwa moja kupitia Viwanda vidogo ambacho kitaanza katika Chuo cha Mafunzo na baadae kwa wananchi

Amesema Viwanda hivyo vitaweza kuzalisha Malighafi au Bidhaa mbalimbali zitazouzwa kwenye sekta ya Utalii pamoja na Matumizi ya ndani kama wananchi mmoa mmoja ambapo kwa sasa hatua inayofuata ni Malighafi za Mkonge kuwasili visiwani Zanzibar baada ya wiki mbili hadi Tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live