Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyavu haramu za Sh170 milioni zateketezwa Rukwa

Nyavu Haram (600 X 338) Nyavu haramu za Sh170 milioni zateketezwa Rukwa

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Nyavu na zana haramu zenye thamani ya Sh170 milioni zilizokuwa zikitumika katika shughuli ya uvuvi ndani ya Ziwa Rukwa zimeteketezwa

Nyavu hizo na zana nyingine haramu zilikuwa zikitumiwa na majangili 481 ambao walikamatwa na kutozwa faini ya Sh246.1 milioni

Meneja wa Pori hilo la Akiba la Uwanda, Orest Njau amesema leo Novemba 8, 2021 kuwa kukamatwa kwa watu hao kunatokana msako ndani ya Ziwa hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Njau amesema kumekuwa na mikakati endelevu ya kudhibiti wavuvi kwenye Ziwa hilo na kuongeza kuwa katika kipindi hicho jumla ya injini 25 za boti na boti 19 zilikamatwa zikiwa zinavua kinyume cha taratibu ya maeneo ya hifadhi hiyo.

Amezitaja zana zingine zilizokamatwa ni pamoja na ngalawa 90, mitumbwi 72, baiskeli 31, mikokoteni miwili na matanki ya mafuta 17.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Sebastian Waryuba amesema kuwa iko haja ya wananchi wa vijiji jirani kuwakumbusha wavuvi wanaovua kwenye Ziwa hilo historia ya muda mrefu ya Ziwa hilo.

Waryuba amesema kuwa iwapo vitendo hivyo haramu vikiendelea samaki ndani ya Ziwa hilo watatoweka na litabaki tupu huku wavuvi waliopo watandoka huku uchumi wa wakazi wa maeneo hayo ya Ziwa Rukwa ukizidi kuporomoka hivyo hawana budi kupinga vitendo vya uvuvi haramu.

Chanzo: mwananchidigital