Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusu wa samaki wa Tanzania wanapoteza ubora wakivuliwa

Wavuvi Mikopo Dawa.jpeg Nusu wa samaki wa Tanzania wanapoteza ubora wakivuliwa

Sun, 14 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri) imesema asilimia 30 hadi 40 ya samaki na dagaa wanapoteza ubora wao na wengine wanaoza wakati wa kuvuliwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tafiri, Dk Ismael Kimirei Mei 11, 2023 amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wawadau wa kuandaa mikakati ya kuondoa upotevu katika sekta ya uvuvi. Dk Kimirei amesema miongoni mwa mikakati yao ni kuwa na teknolojia ambayo itasaidia kuzuia upotevu wa mazao ya uvuvi ikiwemo samaki au dagaa wanapovuliwa wawekwe kwenye barafu kisha wapelekwe mwaloni kwa ajili ya kukaushwa kwenye vyombo maalumu wasipoteze ubora wao.

“Ndiyo maana nchi za wenzetu zilizoendelea wanatembea na barafu wakati samaki na dagaa wanapovuliwa wanawekwa kwenye barafu ili kuzuia kupoteza ubora kwa mazao ya uvuvi lakini hapa Tanzania asilimia 30 hadi 40 samaki au dagaa wanaovuliwa wanaoza na kupoteza ubora wake,”amesem Dk Kimirei. Naye Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) nhini, Charles Tulai amesema wamekutana wadau mbalimbali ili kuandaa mkakati wa kutumia mbinu itakayondoa upotevu katika sekta ya uvuvi hivyo wanatarajia kupata matokeo sahihi. Tulai amesema shirika hilo limeona kuna upotevu mkubwa wa ubora wa samaki na kusababisha kupungua kwa mazao hayo katika mataifa mbalimbali. “Sekta ya uvuvi inaleta ajira hasa katika usindikaji kwa wanawake hivyo ikitumika vizuri utasaidia kuinua kipato na Taifa kwa ujumla,”amesema Tulai. Amesema upotevu wa mazao ya uvuvi umesababishwa na uchafuzi wa mazingira, miundombinu mibovu ambayo imesababisha samaki kupotea hivyo wakiwekeza itasidia upatikanaji mwingi wa zao hilo. Hata hivyo Mtafiti wa ripoti ya upotevu kwa mazao ya uvuvi, Edwin Soka amesema kuna upotevu mkubwa wa samaki na dagaa nchini kwasababu ya kukosekana njia bora za kuvuna mazao hayo na kuyahifadhi. Dk Kimei akizungumzia ulaji wa samaki na dagaa nchini amesema ni asilimia 8.5 kiwango ambacho ni kidogo sana, hivyo kila mtanzania anatakiwa ale kilo 20 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live