Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Nunueni bidhaa zinazozalishwa nchini’

907a016c544a751ae5ab947d1bce9165 ‘Nunueni bidhaa zinazozalishwa nchini’

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JAMII imetakiwa kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na kampuni na viwanda vya ndani ya nchi ili kuviwezesha kuzalisha bidhaa bora zaidi.

Mwito huo ulitolewa na Mwandaaji wa Tuzo za Chaguo la Mteja, Diana Laizer katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa kampuni na watu mbalimbali walioshiriki kwenye utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika juzi, Millennium Tower.

Alisema kwa kununua bidhaa zinazozalishwa nchini, inaongeza chachu ya maendeleo kwa nchi na kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja.

Alisema,”Kwa kuwa serikali hii inasisitizia suala zima la uzalendo kwa watanzania kupenda na kuendeleza vya nyumbani, hakika ni muda sasa wa kuendeleza mapenzi hayo kivitendo kwa kuziunga mkono kampuni za ndani pia.”

Tuzo hizo zilitolewa kwa washindi wa vipengele mbalimbali, ambapo katika kipengele cha tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayofanya vyema kwenye huduma kwa wateja benki iliyoshinda ni CRDB, huku kwa upande wa benki ya kimataifa iliyoshinda ni benki ya Absa.

Kwa upande wa huduma za mawasiliano, Kampuni ya Halotel Tanzania iliibuka mshindi katika kipengele cha kampuni yenye bei stamihilivu za mawasiliano. Katika kipengele cha kampuni yenye mtandao wa kuaminika, ilishinda kampuni ya Vodacom Tanzania.

Upande wa kampuni bora ya bima, iliyoshinda ni Jubilee Insurance huku kampuni bora ya mafuta na petroli ilishinda kampuni ya Lake Oil.

Kampuni ya Nice One ndiyo imeongoza kwa upande wa uzalishaji bora zaidi wa bidhaa za sabuni, kampuni ya HQ imeshinda kuwa kampuni bora ya huduma ya bidhaa za taulo za kike na Sayona imeshinda upande wa uzalishaji bora wa bidhaa za kunywa.

Kampuni ya Air Tanzania imeshinda tuzo mbili, moja ikiwa ya kuwa kampuni ya ndani ya usafiri wa anga inayokubalika zaidi na ya pili kampuni inayokubalika zaidi kimataifa.

Hoteli ya Sea Cliff Hotel Dar imeshinda kipengele cha kampuni inayosifiwa kwa uwezo wake wa huduma bora; huku White Sands Luxury Hotel Zanzibar imeshinda kipengele cha kuwa hoteli inayopendwa zaidi na watalii.

Nao mgahawa wa Grand umeshinda kuwa mgahawa bora unaopendwa zaidi; huku kampuni ya Tour and Travel imekuwa ni kampuni bora ya usafirishaji.

Kampuni iliyoshinda kipengele cha ubunifu wa kidijiti kwenye matangazo, kampuni ya Swahili Digital imeibuka na ushindi huku SGA Security imeshinda kipengele cha kampuni bora ya ulinzi.

Kipengele cha mshereheshaji chipukizi wa mwaka, mshindi ni MC Nguli huku Mshereheshaji wa kike wa mwaka ni Mc Linah na wa kiume akiwa Erick Mchome.

Mpigapicha wa harusi bora mshindi ni Luckson Rugha, mpigapicha bora wa mitindo akiwa Nemy Ngowi na wa matangazo ya biashara ni Nickshine Media Production. Mpigapicha wa matukio aliyeshinda ni Bernard Atilio na mwongozaji bora wa video ni Kenny.

Mwanadada Cherry Suzie ameibuka mshindi kwenye kipengele cha kuwapamba maharusi na mitindo.

Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLeo, HabariLeo Jumapili, Daily News, Sunday News na SpotiLeo ni mmoja wa wadhamini wa shindano hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz