Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nondo, mabati ya Tanzania kuuzwa nje

Mabati Sm Nondo, mabati ya Tanzania kuuzwa nje

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema bidhaa za Nondo na Mabati zinazozalishwa hapa nchini zina ubora wa kuuzwa katika masoko ya kimataifa na hivyo kuwataka watanzania kuzitumia katika shughuli za ujenzi.

Waziri Kijaji ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Viwanda vya Motisun (IMMI Steel) vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo bati, nondo, plastiki, juisi na rangi.

Dkt. Kijaji amesema vipo viwanda nchini vinavyozalisha bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kwamba Watanzania waache kukimbilia nje ya nchi na badala yake wanunue bidhaa zinazozalishwa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live