Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nissan kurejea kwa kishindo

Nissan Z Nissan Z

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni baada ya kampuni ya magari ya Nissan kupitia kipindi kigumu katika miaka michache iliyopita, sasa kampuni hiyo imetangaza kurudi kwa kishindo kwenye biashara ya magari kupitia gari lake jipya la kifahari la Nissan Z.

Baada ya miaka kumi na moja ya uzalishaji wa gari aina ya Nissan 370Z sasa mrithi wake ambaye ni Nissan Z amewasili akiwa na injini ya 400-hp twin-turbocharged 3.0, V-6, Z ambaye alipangwa kuanza kuuzwa Marekani Aprili 2022 lakini ikaahirishwa na sasa gari hili litaanza kuuzwa Marekani kwenye msimu unaofata wa majira ya joto mwaka huu 2022.

Pamoja na kwamba Nissan bado hawajatangaza bei za Z 2023 Wataalamu wanasema huenda bei yake ikaanzia $40,000 ambayo ni zaidi ya milioni 90 za Kitanzania kwa gari hili jipya lenye uwezo wa kubeba Watu wawili. #TanzaniaWeb.Com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live