Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nissan kuongeza nguvu utengenezaji wa magari

NIssan Nissani Nissan kuongeza nguvu utengenezaji wa magari

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nissan inakusudia kuongeza nguvu katika utengenezaji wa magari ya umeme, haswa barani Ulaya ambapo kanuni za uzalishaji wa hewa ukaa ni ngumu zaidi, kampuni hiyo ilisema Jumatatu.

Kampuni ya Nissan Motor Co. imesema katika taarifa kwamba itatoa karibu matoleo yake yote ya Ulaya kuwa ya umeme au mahuluti (hybrids) kwa asilimia 98 ifikapo 2026. Hiyo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 20 kutoka lengo la awali la asilimia 75.

Nchini Japani, kampuni inalenga kutoa asilimia 58 ya matoleo yake yote kuwa ya umeme ikiwa ni ongezeko kidogo kutoka lengo la awali la asilimia 55.

Mahuluti ni mseto wa injini ya petroli na injini ya umeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live