Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yataka ushirikiano zaidi na Tanzania

Nigeria Tanzaniaaaa (600 X 386) Nigeria yataka ushirikiano zaidi na Tanzania

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Nigeria, Kashim Shettima ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi hiyo na Tanzania, akisisitiza uwepo wa juhudi za pamoja ili kufanikisha ukuaji na umoja katika nchi hizo na Bara la Afrika.

Shettima ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na Rais mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Abuja.

Akizungumzia uhusiano wa kihistoria kati ya Nigeria na Tanzania, Makamu wa Rais Shettima amesema nchi hizo zina uhusiano wa muda mrefu hasa kama nchi za mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukoloni.

Ameongeza kuwa Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kupiga hatua kimaendeleo kutoka na kuwa na rasirimali nyingi, jambo ambalo linafungua fursa za ushirikiano wa kina na mafanikio katika ya mataifa hayo mawili na kwamba Nigeria na Tanzania zikipata mafanikio bara zima la Afrika litanufaika.

Kwa upande wake Dkt. Kikwete amesema Tanzania iko tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na Nigeria.

“Tunathamini urafiki na ushirikiano kati ya Nigeria na Tanzania na tumejidhatiti katika kuuimarisha zaidi,” amesema Dkt. Kikwete

Chanzo: www.tanzaniaweb.live