Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nicol yawaagiza wanahisa wake waliofungua kesi kortini kuzifuta

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya uwekezaji Nicol, imetangaza kufuta kesi zote zilifunguliwa na wanahisa kwenye mahakama tofauti nchini.

Uamuzi huo ulitokana na maazimio yaliyopitishwa kwenye mkutano mkuu wa tatu wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika Desemba mwaka jana na kuazimia kufutwa kwa kesi hizo mara moja.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, Nicol imewaandikia barua wanahisa wake wote wenye kesi lakini baadhi ya wanasheria wao hawakuzipokea. Barua hizo zipo tangu Machi 8.

Mwanasheria wa Nicol, Benjamin Mwakagamba aliwataja watu sita ambao hawajachukua barua hizo kuwa ni Felix Mosha, Sylvester Barongo, Dk Bonaventura Mtei, Athony Nyaki, Salum Shamte na Philemon Mgaya na kuwataka kuzichukua ndani ya siku 14 kuanzia juzi (Mei 16) tangazo lililopotolewa kwenye vyombo vya habari. “Hayo ni maelekezo ya mkutano mkuu uliokaa Desemba 2 mwaka jana na kuniagiza nitoe tangazo kwenye magazeti. Baada ya hapo nasubiri maelekezo mengine kutoka kwa wanahisa,” alisema.

Nicol inayomiliki hisa kwenye taasisi nane za zaidi ya Sh97.728 bilioni na amana za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) za Sh30 milioni tangu mwaka 2011, ilianza kuuza hisa zake kwa umma Machi 6, 2004 ili kukuza mtaji.

Kumbukumbu zinaonyesha kampuni hiyo ilifutiwa usajili kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) mwaka 2011, baada ya kushindwa kuchapisha taarifa za fedha kwa miaka miwili mfululizo, mwaka 2009 na 2010.

Licha ya hilo, Nicol ilibainika kufanya baadhi ya uamuzi bila kushirikisha uongozi wa soko hilo kama inavyoagizwa kisheria kwa kampuni zote zilizokamilisha vigezo kwa kushiriki DSE.

Chanzo: mwananchi.co.tz