Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni kweli Tanzania, Kenya zina mafuta ya kutosha?

65e36e81195ba1430f263bb7205dbc17.jpeg Ni kweli Tanzania, Kenya zina mafuta ya kutosha?

Tue, 5 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Kenya Pipeline ya Kenya na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA), zimewahakikishia wananchi uwepo wa akiba ya kutosha ya mafuta katika bohari.

Kwa upande wa Kenya, taarifa ya Kampuni ya Kenya Pipeline imekuja baada ya kuwapo malalamiko kutoka kwa umma kwamba sehemu mbalimbali nchini humo zinashuhudia upungufu wa bidhaa za petroli yakiwamo mafuta ya diezeli, petroli, ya taa na mafuta ya ndege.

Tangu kuibuka kwa vita baina ya Urusi na Ukraine, kumekuwa na hofu kubwa ya kuwapo kwa uhaba wa mafuta kwa kuwa Urusi ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mafuta mengi duniani.

Maeneo yaliyotajwa kuwa na upungufu zaidi Kenya ni Nairobi, katikati mwa nchi, Rift Valley, Nyanza na Magharibi mwa Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mku- rugenzi Mkuu wa Kenya Pipeline, Dk Macharia Irungu, kwa sasa bohari zote za kampuni hiyo zina zaidi ya lita milioni 69 za mafuta ya petroli aina ya ‘super’, zaidi ya lita milioni 64 za mafuta ya dizeli, zaidi ya lita milioni 13 za mafuta ya taa na zaidi ya lita milioni 23 za mafuta ya ndege.

Irungu aliwahakikishia Wakenya kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kusambaza mafuta.

Nchini Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Ewura, Godfrey Chibulunje alisema mwishoni mwa wiki kuwa serikali inachukua hatua zote madhubuti kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha.

Kwa mujibu wa Ewura, Tanzania ina mafuta ya akiba ya kutosha takribani siku 30 zijazo na kwamba, meli nyingi zilizopakia mzigo wa mafuta ziko njiani kuja Tanzania.

“Tanzania ina hifadhi ya petroli ya kutosha inayoweza kutumika kwa siku 27, dizeli hadi siku 19 na mafuta ya taa kwa siku 114, hii ni kuwahakikishia kuwa hakuna uwezekano wa kukosekana kwa mafuta hivi karibuni,” alisema Chibulunje.

Chibulunje aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari kuwa meli zilizosheheni mafuta ziko njiani kuja Tanzania na tayari serikali imetoa oda katika nchi za Uarabuni ili mzigo zaidi wa mafuta ufike baadaye.

Pamoja na kuwapo uwezekano wa kupanda kwa bei ya mafuta, wananchi nchini Kenya na Tanzania wanaziomba mamlaka kudhibiti mfumo holela wa bei za bidhaa na huduma ili kuwapunguzia makali ya maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live