Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguvu kuongezwa uzalishaji ngano nchini

Ngano Ngano Nguvu kuongezwa uzalishaji ngano nchini

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya nafaka na mazao mchanganyiko (COPRA), Imeingia makubaliano na taasisi zinazohusiana na usambazaji, usindikaji na uchakataji wa zao la ngano nchini ambapo wamesaini makubaliano na Mkurungenzi wa Mamlaka hiyo, Irene Mlola katika viwanja wa Nane nane Nzuguni Jijini Dodoma.

Hafla ya utiaji saini imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (Mb) ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wakuu wa Taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi nao pia walishiriki.

Akizungumza katika hafla Hiyo Naibu waziri Silinde ameipongeza COPRA kwa kusaini makubaliano hayo ambayo yatakwenda kuongeza chachu ya uzalishaji wa zao la ngano hapa nchini.

Aidha Mhe. Silinde Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono ya dhati kwa vitendo katika kukuza sekta ya kilimo ambapo masoko ya kimataifa yamefunguka kwa kiwango kikubwa hivyo wakulima wajikite kwa uzalishaji wa zao hilo la Ngano.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa COPRA, Irene Mlola amezipongeza kampuni zote walizoingia nazo makubaliano ambao ni wasambazaji, Wasindikaji na wachakataji kwa pamoja watakwenda kununua Zao hilo kutoka kwa wakulima hivyo itapelekea wakulima kuuza kwa bei nzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live