Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro yawakosha watalii..

Ngorongoro Crater Tanzania Safari 1 Scaled.jpeg Ngorongoro yawakosha watalii..

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa kawaidia Tanzania imekuwa ikipokea wageni kutoka mataifa mbalimbali Duniani kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii,Watalii wanaotembelea vivutio vya Utalii nchini hususan eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wameendelea kuvutiwa na aina mbalimbali za shughuli za utalii zilizoko katika Hifadhi hiyo.

Shughuli za utalii ambazo zinafanyika katika hifadhi ya Ngorongoro ni pamoja na utalii wa picha (Photographic tourism), utalii wa kutembea (walking safaris), Utalii wa akiolojia (archeological tourism) katika Bonde la Olduvai na Laetoli, utalii wa kupanda maputo angani (hot air balloon) na utalii wa kupanda milima (Mountain hiking) ambayo vyote vinapatikana katika hifadhi ya Ngorongoro.

Remen Rudolff kutoka Marekani ameelezea kufurahishwa na utalii wa picha katika bonde la Ngorongoro lenye umbo la kipekee la mandhari asilia yaliyopambwa na mtawanyiko wa wanyama na ndege mbalimbali.

Taarifa kutoka kwa Uongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt. Freddy Manongi kati ya mwezi Julai 2022 hadi Juni 2023 jumla ya watalii 752,232 walitembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, hii ni tofauti na mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo jumla ya watalii walikuwa 425,386.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live