Menu ›
Biashara
Mon, 6 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ili kuongeza tija katika biashara ya mifugo, Serikali imeanza kuweka mizani katika minada ya ng'ombe ili waanze kuuzwa kwa kilo badala ya makisio.
Hayo yamesema leo Februari 6, 2023 katika ya hafla ya kupokea mizani 82 ambayo itasimikwa katika baadhi ya minada ya mifugo iliyopo katika Mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema mizani hizo zimegharimu Sh249.27 milioni huku akitaka minada yote ya mifugo kuweka mizani ili kuongeza ushindani.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live