Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nemc yafunga machinjio ya Msalato

82426 Nemc+pic Nemc yafunga machinjio ya Msalato

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini Tanzania (Nemc) limeifunga machinjio ya Msalato na kuitoza Halmashauri ya Jiji la Dodoma faini ya Sh5 milioni.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara katika machinjio hiyo.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 31,  2019 mkurugenzi mkuu wa Nemc,  Dk Samwel Gwamaka amesema hawataifungua hadi watakapojiridhisha kuwa imetimiza vigezo.

"Machinjio hii inahatarisha afya za walaji pamoja na kuifungua watalipa faini ya Sh5 milioni," amesema Dk Gwamaka baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na naibu  Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima.

Ofisa wa Mifugo mjini Dodoma, Gration Mwesiga amesema katika machinjio hiyo mbuzi wanaochinjwa ni kati ya 10 hadi 20, ng’ombe  10 hadi 20 siku za mnada Jumamosi.

Amesema katika mwaka wa fedha 2019/ 20 wametenga Sh50 milioni kwa ajili ya ukarabati wa machinjio hiyo. Naye mbunge wa Igalula (CCM), Mussa Ntimizi amesema endapo walaji wa nyama wangefika katika machinjio hiyo na kuona uchafu uliopo wasingerudi tena kununua.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz