Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neema yaviangukia vyuo vya uvuvi

Neema yaviangukia vyuo vya uvuvi

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

T: Neema yaviangukia vyuo vya uvuvi

S: Angalau vijana zaidi ya 200 kati ya  420 waliokosa udahili katika vyuo vya mifugo na uvuvi vya mkoani Mara na Mtwara, sasa watapata ahueni baada ya Serikali kutoa Sh200 milioni kwa vyuo hivyo.

Mara. Angalau vijana zaidi ya 200 kati ya  420 waliokosa udahili katika vyuo vya mifugo na uvuvi vya mkoani Mara na Mtwara, sasa watapata ahueni baada ya Serikali kutoa Sh200 milioni kwa vyuo hivyo.

Awali,  vijana hao walikosa nafasi baada ya vyuo hivyo kutokuwa na miundombinu stahiki ya kudahili wanafunzi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina alisema sekta ya uvuvi ina umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla, lakini vijana wengi hawana elimu ya kutosha juu ya namna ya kuboresha shughuli zao. Aliagiza uongozi wa vyuo hivyo kuhakikisha kuwa wanafanya maboresho ya miundombinu katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa mabweni ili kuweza kuwadahili vijana hao mapema Januari mwakani. "Najua mtajua namna ya kufidia muda huu uliopotea mtakapowadahili wanafunzi mwezi ujao kuliko kukaa na kusubiri mwaka mwingine wa masomo. Kwa hiyo nataka mhakikishe kazi zinafanyika usiku na mchana ili kundi hili la vijana lianze masomo haraka iwezekanavyom” amesema Waziri Mpina. Wakizungumzia uamuzi huo, baadhi ya vijana kutoka katika kijiji cha Gabimori mkoani Mara walisema kuwa uamuzi huo umekuja muda mwafaka na kwamba utasaidia kuongeza nafasi za ajira kwa vijana. Mwita Webiro alisema vijana wengi hawana ajira nchini kutokana na kutokuwapo kwa ajira katika sekta rasmi lakini kuwapo kwa vyuo hivyo kutasaidia vijana wengi kujijajiri. Alisema kuwa vijana wengi wakipata nafasi ya kujifunza kwa nadharia juu ya ufugaji wa samaki, upo uwezekano mkubwa wa kujiajiri na hatimaye kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato.

Chanzo: mwananchi.co.tz