Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neema ya ajira sekta ya anga Kusini mwa Afrika

Ndege Rt Neema ya ajira sekta ya anga Kusini mwa Afrika

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati ripoti ya tovuti maarufu ya usafiri wa anga ya ‘Aviation Benefits Beyond Boarders’ ikionyesha sekta hiyo katika bara la Afrika hadi mwaka 2018 ilitoa ajira milioni 7.7, shirika la ndege ya Air France imepanua huduma zake hadi nchi 31 kusini mwa jangwa la sahara.

Hatua hiyo yenye lengo la kuboresha huduma za anga inatajwa kusaidia kuongeza ajira kwa wakazi wa eneo hilo kwa ujumla lakini pia matumizi ya teknolojia rafiki yanatajwa kusaidia utunzaji wa mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Air France KLM inayomiliki shirika hilo, kwa Afrika Mashariki na Kusini, Nigeria, na Ghana, Marius van der Ham, katika maadhimisho ya miaka 90 ya shirika la Air France katika usafiri wa anga amesema hatua hiyo mbali na kuchangia uchumi lakini pia itaboresha ustawi wa abiria na mazingira.

"Tutaendelea kuvumbua na kuinua viwango vyetu, tukihakikisha uzoefu wa usafiri usio na kifani ambao unatanguliza ustawi wa abiria na kuridhika,"amesema.

Van der Ham ameongeza kuwa huduma za kibunifu zinapewa kipaumbele, na shirika linazingatia kuboresha uzoefu wa jumla wa abiria, ikiwa ni pamoja na michakato iliyoratibiwa ya kuhifadhi na huduma za kibinafsi za ndani ya ndege.

“Abiria wa Air France wanaosafiri kati ya Afrika wataendelea kufurahia huduma za hivi punde, vyumba vikubwa, na chaguzi za burudani zinazofanya safari kuwa uzoefu wa kufurahisha,”amesema.

Mbali na hufuma za anga, shirika hilo pia linafanya jitihada katika kutunza mazingira huku likiwa na nia ya kupunguza kiwango chake cha kaboni.

“Katika upande wa teknolojia tuchagua ndege zile zenye sifa nzuri za urafiki wa mazingira na uzalishaji mdogo. Hii ni hatua muhimu kuelekea malengo ya kudumisha mazingira,”amesema Van der Ham.

Mdau wa Mazingira, Alex Mnyinda amesema hatua ya shirika hilo kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa njia ya teknolojia ni mfano wa kuigwa kwa kampuni nyingine ili dunia iwe sehemu salama.

“Siku zote wadau wa mazingira tunakuwa mstari wa mbele kuzikumbusha kampuni kubwa na nchi zenye viwanda vingi kuhakikisha wana mpango madhubuti wa kupunguza athari za kaboni, mpango wa Air France ni wa kuigwa,”amesema Mnyinda.

Naye Mchambuzi wa masuala ya Uchumi, Mack Patrick amesema kupanua huduma katika nchi 31 inamaanisha uchumi wa nchi hizo zilizoguswa utaongezeka kutokana na fursa mbalimbali ikiwamo ajira.

“Kwa lugha nyepesi tu, ajira ndio kitu cha kwanza tunakiangalia katika utendaji kazi wa kampuni kubwa kama ile, lazima wananchi watafaidika,”amesema Mack.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live