Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro asisitiza demokrasia ya uchumi

716b97b54efdb407eabad03c5a436e44 Ndumbaro asisitiza demokrasia ya uchumi

Sat, 29 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuweka nguvu katika Diplomasia ya Uchumi ikiwemo kuwavutia watalii kutoka nje.

Dk Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Januari 29, 2022 wakati wa ziara ya kutembelea ofisi ya Ubalozi huo ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na Watumishi na Wawekezaji mara baada ya mkutano wa 50 wa mwaka wa uwindaji wa kitalii uliofanyika katika Jiji la Las Vegas nchini Mareakani.

Akizungumza na timu ya Watumishi hao, Dk Ndumbaro amempongeza Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Dk Elsie Kanza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Diplomasia katika tasni ya biashara na utalii.

Amesema wanadiplomasia hao wanapaswa kutangaza na kujibu maswali ya watu mbalimbali wanaotaka kutalii Tanzania kuhusu namna ya kufika nchini kiujumla na katika kila kivutio cha utalii kimahususi.

"Kutokana na kasi kubwa ya maendeleo ya kiuchumi, Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi Diplomasia ya kiuchumi ndo injini ya maendeleo haikwepi, ongezeni ujuzi katika eneo hilo." amesisitiza Dk Ndumbaro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live