Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndizi za Tanzania bara zaruhusiwa kuuzwa Zanzibar

Ndizi Mbivuuuuuuu Ndizi za Tanzania bara zaruhusiwa kuuzwa Zanzibar

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Zanzibar imeruhusu uingizwaji wa zao la ndizi Nchini humo zinazotoka Tanzania Bara baada ya kuzuia tangu mwaka 2017 ambapo imesema licha ya kuruhusu itachukua tahadhari juu ya magonjwa mbalimbali yanayoathiri zao hilo.

Akitangaza uamuzi huo leo March 15,2024 Visiwani Zanzibar, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis amesema mwaka 2007 Serikali ya Zanzibar ilitangaza marufuku ya kutoingiza mmea wa migomba na mazao yake zikiwemo ndizi kwa lengo la kuikinga Zanzibar isishambuliwe na maradhi ya mnyauko wa migomba yaliyoonekana katika maeneo ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Kagera, Bukoba na Mara.

“Nataka niwaambie kuwa tahadhari iliyowekwa imepelekea kuwa na uhaba mkubwa wa ndizi kwa kipindi cha miaka 17 jambo ambalo limesababisha changamoto mbalimbali kwa Wakaguzi wa mazao, Wafanyabiashara na Wadau wengne katika utekelezwaji wa tahadhari hiyo”

Amesema Serikali inaruhusu uingizwaji wa zao la ndizi kwa mujibu wa sheria ya karantini ya mmea na mazao namba 9 ya mwaka 1997 kwa utaratibu maalum ili kupunguza changamoto iliyojitokeza “Wafanyabiashara wanaoruhusiwa kufanya biashara ya ndizi wanatakiwa kusajiliwa na kupatiwa vibali maalum vya uingizwaji wa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo na kupeleka bidhaa hizo kwa Wakaguzi wa Kitengo cha Karantini na Ukaguzi wa Mazao kabla hazijaingia kwenye masoko”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live