Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege zisizo za rubani kusajiliwa kwa Dola 100

7ca80470987bff98b4c71087f0245279 Ndege zisizo za rubani kusajiliwa kwa Dola 100

Wed, 2 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetangaza kuwa gharama za kusajili ndege zisizo na rubani (drones) ni Dola za Marekani 100 sawa na Sh 231,992 za Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari kwa vyombo vya habari, mamlaka hiyo iliagiza tangu Agosti 23, mwaka huu, kwa vyombo hivyo kuhusu ukomo wa matumizi ya ndege hizo bila usajili.

Alisema agizo hilo lilihusu ndege ambazo zilipewa kibali awali na ambazo hazijasajiliwa ikiwa ni utekelezaji wa kanuni za kiusalama za kudhibiti matumizi ya ndege zisizo na rubani za mwaka 2018.

Aliwataka wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha wanafuata hatua zote za usajili ikiwemo kulipa gharama hizo za usajili ambazo hulipwa mara moja tu.

“Usajili utafanywa mara moja tu kwa kila ndege, hivyo mmiliki halazimiki kusajili au kuhuisha usajili wa ndege yake kila mwaka,”ilieleza taarifa ya Johari.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, miongoni mwa hatua za usajili kuwa ni kukamilisha nyaraka zote za usajili zinazohitajika zikiwemo fomu, barua na mwongozo wa utumiaji, mamlaka kughulikia nyaraka hizo na kufanya upekuzi kupitia vyombo vya usalama na mtumiaji kupatiwa cheti cha usajili.

Aidha, hatua nyingine ni kuhakikisha chombo kinapatiwa kibali cha matumizi kila kinapohitaji kutumia ndege hiyo kwa kuwasilisha fomu ya maombi na nakala ya cheti cha usajili wa ndege ambapo hakutakuwa na malipo yeyote katika kuomba kibali wala upekuzi.

“Mbali na kibali mtumiaji anapaswa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na serikali za mtaa katika eneo analotaka kufanyakazi yake,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Johari kila mtumiaji anapohitaji kutumia ndege hizo anapaswa kuomba kibali cha mamlaka baada ya kuanisha eneo la kazi, kazi yenyewe na muda wa kazi.

Ilieleza kuwa, hatua hiyo itasaidia TAA kutambua na kufuatilia mahali ilipo ndege kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa watumiaji wengine wa anga.

“Muombaji anapaswa kutumia ndege yake katika maeneo ay mkoa iliyoidhinishwa nayo na endapo muombaji atataka kufanya matumizi nje ya maeneo au mikoa iliyoidhinishwa atatakiwa kuomba kibali kingine bila gharama yeyote,” ilieleza taarifa hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz