Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege za Tanzania kuanza safari za India, China

46311 PIC+INDIA Ndege za Tanzania kuanza safari za India, China

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk Philip Mpango amesema Serikali iko mbioni kuanza kurusha ndege zaka katika nchi za India na China.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 12, 2019 wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa maendeleo wa taifa ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/20

Amesema kuanzishwa kwa safari hizo kunatokana na ununuzi wa ndege nyingine ikiwa ni mkakati wa kukamata masoko mapya ya utalii.

"Hatua iliyofikiwa ni kuwasili kwa ndege nyingine tatu, moja ikiwa ni Boeing 787-8 dreamliner na mbili zikiwa ni Airbus A220-300, hivyo kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa kuwa sita," amesema Mpango.



Chanzo: mwananchi.co.tz