Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya mizigo ya ATCL kufanya safari ya pili leo

ATCL Ndege Cargo.png Ndege ya mizigo ya ATCL kufanya safari ya pili leo

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo Jumatatu, Julai 10, 2023 inatarajia kufanya safari yake ya pili ya kupeleka mzigo Dubai huku ikiendelea kuvutia kasi masoko mengine muhimu.

Julai 7, 2023 ndege hiyo aina ya Boeing 767-300F ilifanya safari yake ya kwanza kwenda Dubai ikitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julias Nyerere (JNIA).

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo, Patrick Ndekena alisema ratiba ya safari za Dubai itakuwa mara mbili kwa wiki (Ijumaa na Jumatatu).

Alisema adhma ya ATCL ni kuhakikisha bidhaa za wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi zinafika kwa wakati na zikiwa na ubora wake kwenye nchi mbalimbali kwa kadri ya inavyotakiwa.

“Leo tunafuraha kubwa kwa kuanza rasmi safari zetu za ratiba kwa ndege yetu hii mpya ya mizigo Boeing 767-300F yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu na uzito mkubwa yaani tani 54 kwa mara moja,” alisema Ndekena wakati ndege hiyo ikipakia mzigo kwa mara ya kwanza.

Akifafanua kuhusu uwezo wa ndege hiyo alisema nitoleo la kisasa, ina uwezo wa kwenda mwendo wa kilometa 850 kwa saa na kukaa angani kwa zaidi ya masaa 10 bila kutua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live