Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya mizigo kuanza kazi wiki ijayo

ATCL ATCL CARGO.jpeg Ndege ya mizigo kuanza kazi wiki ijayo

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NDEGE mpya ya mizigo aina ya Boeing 767-300F iliyonunuliwa na serikali itaanza kazi ya kusafirisha mizigo nje ya nchi Juni 26, mwaka huu. - Hayo yalibainishwa na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Sarah Reuben alipozungumza na HabariLEO. - Reuben alisema kuanzia Jumatatu ijayo, ndege hiyo itaanza kusafirisha mizigo kwenda kwenye miji ya Mumbai nchini India, Kinshasa na Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na nchini Dubai. - “Tunayo furaha kutangaza huduma zetu za kusafirisha mizigo kwenda Dubai, Mumbai, Kinshasa na Lubumbashi ambazo zitaanza Juni 26, mwaka huu,” alisema. - Kutokana na kuanza kwa safari hizo, alitoa wito kwa wafanyabiashara kufikia viwango vipya katika biashara zao kimataifa kwa kutumia ndege hiyo ya mizigo ya ATCL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live