Ndege ya mizigo ya Air Tanzania (Air Tanzania Cargo) imeshusha mzigo wa magari Kenneth Kaunda Aiport, Lusaka nchini Zambia ambao umesafirishwa kutoka Dubai kupitia Tanzania hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa ndege hii kusafirisha magari.
Gerald Mbago ni Afisa anayehusika na upangaji wa mizigo ndani ya Air Tanzania Cargo ambapo amesema licha ya uwepo wa safari za ratiba, ATCL imeendelea kusafirisha mizigo ya Wafanyabiashara, Taasisi za Kimataifa, Kampuni pamoja na watu binafsi kwa kukodisha ndege na kupeleka katika maeneo wanayohitaji huduma hiyo kama ilivyosafirisha magari hayo.
Air Tanzani Cargo iliwasili June mwaka huu na kuanza shughuli zake mwezi July ikisafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nchini Tanzania kwenda kwenye masoko mbalimbali ya Kimataifa na kutoka Nchi za nje kuleta nchini Tanzania.