Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya Uswisi Yatua Tanzania Kuanza Safari Zake

Tourist Data Ndege ya Uswisi Yatua Tanzania Kuanza Safari Zake

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ndege aina ya Airbus A343 ya Shirika la Ndege la Uswisi EDELWEISS, imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) ikiwa na watalii 260 kutoka Uswisi. Tukio hilo ni uzinduzi Safari za moja kwa moja za Ndege za Eldewiss, kutoka Uswisi kuja Tanzania.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa, kwa pamoja na Balozi wa Uswisi nchini Didier Chasot, baada ya Ndege hiyo kuwasili Uwanjani hapo majira ya saa 1:40 asubuhi, atakata utepe kuashiria kuanza kwa safari za Ndege za Moja kwa moja za Eldewiss, nchini Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Kilimanjaro ( KADCO), atakuwa sambamba na wageni Wa hafla hiyo.

Miongoni mwa Faida za Ruti ya Ndege hiyo, ni kuongeza Makusanyo katika Uwanja wa Ndege wa KIA, kuongeza makusanyo kwa wadau ambao ni Sekta ya Anga na Utalii, Aidha ni kuunga mkono malengo ya Serikali, kuvutia Watalii Milioni 5 Ifikapo mwaka 2025.

Ndege hiyo inatarajiwa kuruka KIA, majira ya Saa3:10 asubuhi kuelekea Zanzibar.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Chanzo: globalpublishers.co.tz