Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya KQ yalazimishwa kurudi Afrika Kusini baada ya kumsahau fundi ndani

83254 KQ+PIC Ndege ya KQ yalazimishwa kurudi Afrika Kusini baada ya kumsahau fundi ndani

Sun, 10 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Ndege ya Boeing 787 inayomilikiwa na Kampuni ya Ndege ya Kenya (KQ) imelazimika kurudi jijini Johannesburg, Afrika Kusini baada kubani kuwa kuna mtu amesahaulika.

Mtu huyo ambaye kitaaluma ni fundi wa ndege anasadikiwa aliingia katika moja ya vyumba vya chini vinavyopatikana katika ndege hiyo na ilipoanza safari hakuonekana.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Johannesburg kwenda Nairobi, Kenya ilirejea nchini Afrika Kusini dakika 30 baada ya kupaa.

Hata hivyo, tukio hilo limeibua maswali katika mitandao ya kijamii ambako watumiaji wake wamehoji mambo kadhaa ikiwamo mtu huyo alikuwa wapi, nani aligundua uwepo wake katika ndege hiyo, alitokaje na rubani alipata taarifa vipi?

Inaelezwa kuwa muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa rubani wa ndege hiyo alilazimika kurejea Afrika Kusini baada ya kugundua kuna mtu amesahaulika ndani.

Taarifa zaidi zinasema kuwa fundi huyo aligunduliwa baada ya ndege hiyo kutua nchini Afrika Kusini.

“Yuko hapa salama na anajitambua,” alinukuliwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo.

Mpaka sasa haijajulikana sababu ya fundi huyo kusahaulika ndani ya ndege hiyo huku wengine wakidhani kuwa alikuwa mzamiaji.

Hata hivyo, Kampuni ya KQ haijathibitisha madai ya mtu huyo kuwa mzamiaji.

Kwa mujibu wa tovuti ya Gazeti la The Daily Nation la Kenya, ndege hiyo ilibaki ardhini kwa muda wa saa moja baada ya kumshusha mtu huyo.

Taarifa za safari zilionyesha kuwa ndege hiyo iliondoka tena nchini Afrika Kusini saa 7.35 na kutua jijini Nairobi baada ya kucheleweshwa kwa dakika 105 sawa na saa 1.45

Hii sio mara ya kwanza kwa ndege za KQ kupatwa na majanga ya namna hiyo, Juni mwaka huu mwili wa mwanaume ulianguka kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow jijini London, Uingereza.

Ndege hiyo ya KQ 100 ilikuwa ikisafiri kutoka jijini Nairobi kuelekea mji mkuu wa Uingereza.

Hata hivyo, mwili huo haukuweza kutambuliwa na badala yake wapelelezi walibaini uwapo wa begi dogo lililokuwa na chakula na nguo ambalo lilifichwa katika eneo la gia ya (tairi) nyuma ya kutua. Oktoba mwaka huu Jeshi la Polisi nchini Uingereza lilitoa mchoro wa tukio hilo na kuomba ushirikiano kwa mtu anayeweza kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz