Serikali imesema muda wowote kuanzia sasa ndege mpya ya mizigo inatarajiwa kuwasili nchini ikiwa ni kati ya ndege mpya tano zikiwemo za abiria zilizopangwa kununuliwa na Serikali.
Akizungumza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), John Nzulule amesema tayari amewasiliana na Kampuni ya Boeng ya nchini Marekani na ikawaeleza kuwa muda wowote kuanzia sasa ndege hiyo itakuwa tayari kukabidhiwa.
“Timu ya Tanzania ya mwisho kwenda kukagua itakuwa tayari wakati wowote kufanya hivyo, na habari zaidi tutawajulisha,” amesema Nzulule.
Hata hivyo mwezi Februari mwaka huu, Nzulule alisema ndege hiyo itawasili nchini kati ya mwezi Machi au Aprili mwaka huu huku ndege nyingine zinatarajiwa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti ndani ya mwaka huu.