Naibu WazirI wa Uchukuzi David Kihenzile ameitaka kampuni ya Ndege ya ATCL kuendelea kuandaa mpango na mapokezi ya ndege mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini mapema 2024 ambazo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua ili kuongeza mzunguko wa safari za Ndege Nchini.
Kihenzile amesema kuwa Rais Samia ameona umuhimu wa kuongeza Ndege zingine nchini hivyo ameamua kuagiza ndege zingine mbili za masafa ya Kati moja 737-9 Boeing inayotarajiwa kuwasili mwezi Januari 2024 na ya pili ni ya Masafa marefu aina ya Boeing 737-8 Inayotarajiwa kuwasili mwezi March 2024.
Kihenzile ameyasema hayo alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amekiri kupokea malalamiko ya mara kwa mara ya wasafiri ya kuahirisha safari za ndege zake kunakochangiwa na uhaba wa ndege zilizopo huku zingine zikiwa kwenye matengenezo.