Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege kubwa ya Ureno yawasili Zanzibar

Ureno Ndege Kubwa.png Ndege kubwa ya Ureno yawasili Zanzibar

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mara ya kwanza imepokea ndege ya safari ya moja kwa moja kutoka nchini Ureno ikiwa ni sehemu ya kuimarisha sekta ya utalii Visiwani Zanzibar

Waziri wa Ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar Dkt Khalid Salum ameongoza mapokezi ya ndege aina ya HiFly kutokea nchini Ureno ikiwa na abiria mia mbili themanini na nane (288) ambapo hatua hiyo inatajwa kuchochea uchumi wa Zanzibar

Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Simai Mohammed Said amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuekeza nguvu kubwa katika kuiwezesha wizara hiyo kutanua wigo wa kutafuta masoko kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni

Chanzo: www.tanzaniaweb.live