Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege kubwa kuanza kutua Tanga

Atcl Atcl.jpeg Ndege kubwa kuanza kutua Tanga

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewahakikishia Wananchi wa Tanga kusudio lake la kukiboresha kiwanja cha ndege cha Jiji hilo hususani katika jengo la abiria, maegesho ya ndege, na eneo la kuruka na kutua ndege ili kuendana na mahitaji ikiwemo kuruhusu ndege kubwa kutua.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema hayo baada ya kutembelea Tanga Airport na kuona uhitaji wa maboresho hayo.

“Ukiangalia tumekaa kwa kipindi kirefu hakujawahi kufanyika mabadiliko yoyote katika Airport hii hivyo Rais Mh. Samia ameona ni muhimu kufungua Mkoa wa Tanga kwenye upande wa usafiri wa anga kwa kuhakikisha ndege kubwa zinatua hapa na uwepo wa Airport ya kisasa ndani ya Jiji la Tanga”

Naibu Waziri amesema uboreshaji wa Airport hiyo, utaenda sawa na mahitaji ya sasa na fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga ikiwa ni pamoja na fursa ya uwekezaji wa bomba la mafuta ambalo litaongeza idadi ya Wageni watakaohitaji kutumia usafiri wa aina mbalimbali ukiwemo usafiri wa anga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live