Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ATR 72-500 ya Precision kutua nchini

Precision Air ATR 42 600 (5H PWH) Ndege ATR 72-500 ya Precision kutua nchini

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

hirika la ndege la Kitanzania Precision Air, limesema kwamba linatarajia kuongeza ndege mpya aina ya ATR 72-500 yenye uwezo wa kubeba abiria 72.

Ndege hiyo inatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumamosi Tarehe 21 Oktoba 2023. Nakuanza kufanya safari mara moja wiki inayofuatia baada ya kukamilisha taratibu za usajili.

Meneja Masoko na Mawasiliano Bw. Hilary Mremi amesema, Precision Air imechagua kuongeza ndege nyingine aina ya ATR-72 -500 kwasababu aina hiyo ya ndege imethibitisha kua chaguo sahihi kwa mazingira ya Tanzania na safari za kikanda.

“Ndege hii imekuja wakati muafaka kwa ajili ya kuhudumia ongezeko la soko linalo tarajiwa wakati wa msimu wa sikukuu. Precision Air imejidhatiti kutoa huduma bora na za uhakika na kupitia ongezeko hili la ndege tunawahakikishia abiria wetu huduma bora.”

Ameongeza kuwa tayari tiketi za msimu wa sikukuu zinapatikana kupitia tovuti ya Precision Air au Whatsapp ( Bwana Swala) na wateja wanaweza fanya booking zao sasa.

Precision Air ni shirika la Kitanzania lililo na makao yake makuu Jijini Dar es Salaam na kufanya safari kwende maeneo zaidi ya 13 ndani na nje ya nchi. Kutokea Dar es Salaam Precision Air inasafiri kwenda, Arusha, Bukoba,Mbeya, Mwanza,Mtwara, Kahama, Kilimanjaro,Zanzibar,Nairobi,Hahaya, Anjouan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live