Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndalichako awataka wawekezaji sekta ya viwanda kuzingatia sheria

NDALICHAKOOOO Ndalichako awataka wawekezaji sekta ya viwanda kuzingatia sheria

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako amewataka wawekezaji wa sekta ya viwanda kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali ya kazi nchini, ikiwemo kuboresha mifumo ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi ilikuwalinda wafanyakazi dhidi ya athari wanazoweza kuzipata wakiwa kazini.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maenedeleo ya Jamii ya kutembelea viwanda Mkoani Arusha akiambatana na kamati hiyo ili kujionea utekelezaji wa sheria na miongozi mbalimbali ya kazi ikiwemo Sheria Na.5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Riziki Saidi Lulida amewataka wawekezaji hao kuhakikisha wanaweka miundo mbinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali ya viwanda vyao ili kurahisisha shughuli mbalimbali zinazoweza kufanywa na wenye ulemavu.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Jang’ombe, Mhe. Ali Hassan King ameishauri taasisi ya OSHA kuendelea kuimairisha mifumo ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi huku Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi wa OSHA, Dkt. Jerome Materu akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa OSHA amewasihi wawekezaji hao kuwekeza kikamilifu katika masuala ya usalama na afya ili kupunguza gharama za uendeshaji wa viwanda vyao.

Katika ziara hiyo Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imetembelea viwanda vitatu Mkoani Arusha ambavyo ni Kiwanda cha kuzalisha Transifoma cha TANELEC Limited, Kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo cha A to Z Textiles Mills Ltd pamoja na kiwanda cha maua cha Fides Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live