Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za EAC kuoanisha gharama za simu

65129 Pic+eac

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Watumiaji wa mitandao ya simu za kiganjani wataanza kupata nafuu ya kupiga simu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Serikali ya Tanzania kuanza mchakato wa kutekeleza mkataba wa EAC wa kuoanisha gharama hizo miongoni mwa nchi wanachama.

Akizungumza jijini Mwanza leo Jumatatu Julai Mosi, 2019, Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Atashasta Nditiye amesema mchakato huo utakamilika muda wowote kuanzia sasa.

Naibu Waziri huyo alikuwa anafungua mkutano wa siku tano wa wataalam wa mawasiliano kutoka mamlaka za mawasiliano za wanachama wa EAC.

Tanzania na Burundi ndizo nchi pekee kati sita wanachama wa EAC ambao hawajakamilisha mchakato huo.

Nchi za Kenya, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini tayari zimeoanisha gharama za simu ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa EAC kuhusu sekta ya mawasiliano ya simu.

"Tuko hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuoanisha gharama za kupiga simu miongoni mwa nchi wanachama wa EAC," amesema Nditiye

Pia Soma

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amewaeleza washiriki kuwa licha ya Tanzania kutokamilisha mchakato huo, sera za mawasiliano nchini ndizo zilizo bora kulinganisha na mataifa mengine wanachama wa EAC.

Amesema sababu zinahusisha huduma na manufaa kwa asilimia 94 ya wananchi wote hadi vijijini.

"Sera za Tanzania ndizo zimeigwa na EAC kutokana na ubora wake na upatikanaji wa mawasiliano vijijini," amesema Kilaba

Kwa upande wake, Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano wa EAC, Ally Simba amesema lengo la kuoanisha gharama za mawasiliano miongoni mwa raia wa nchi wanachama kurahisisha mawasiliano.

Chanzo: mwananchi.co.tz