Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi tatu kununua chakula Tanzania

Mahindi Pic Data Nchi tatu kununua chakula Tanzania

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imetangaza kuwa nchi za Zambia, Malawi, Msumbiji zinahitaji chakula, hivyo wafanyabiashara wachangamkie fursa ya kuuza mazao huko. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amehimiza wafanyabiashara wazitumie balozi za Tanzania katika nchi hizo, wakatafute mikataba na wizara itawapa ushirikiano.

“Msisubiri waje hapa, tokeni nje, soko la Kenya matarajio yetu litachelewa kuanza mpaka mwezi JulaiAgosti na hili tunashindana na Uganda. “Malawi na Mozambique (Msumbiji) mwaka huu napo kuna upungufu wa mahindi na taswira hii inaonesha kuwa fursa ni kubwa,” aliandika Bashe katika ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa X akitoa taarifa fupi ya uzalishaji mazao katika msimu wa kilimo 2022/23.

Alieleza kuwa katika msimu huo, taifa lilizalisha mahindi zaidi ya tani milioni 8.1 na mahitaji ya nchi ni tani zisizozidi milioni sita na kwa muda mrefu mazao yamekuwa yakipelekwa Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rwanda. Bashe alieleza kuwa tathmini ya awali nchi hizo ukiondoa Kenya zinahitaji zaidi ya tani milioni 1.2 na akahimiza wafanyabiashara wanapokwenda huko wazingatie sheria za nchi husika. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, dhamira ya serikali ni biashara ya mazao ifanywe na sekta binafsi zaidi badala ya serikali kwa serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live