Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi saba zajadili maono sekta ya madini

56511 MADINI+PIC

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Viongozi, wataalamu katika sekta ya madini kutoka nchi saba za Afrika wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili namna ya uwezeshaji wa maono ya Afrika katika sekta ya madini Tanzania.

Jukwaa hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Uongozi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Wizara ya Madini nchini.

Viongozi na wataalamu hao ni wa sekta binafsi na umma, asasi za kiraia, wanawakilisha wa nchi za Botswana, Nigeria, Kenya, Ghana, Uganda, Lesotho na mwenyeji Tanzania.

Akizungumza na wanahabari, leo, Alhamisi Mei 9,2019, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja amesema, “washiriki wataeleza uzoefu wao, watajadili kikamilifu mbinu zitakazosaidia kuiwezesha nchi katika umiliki wa sekta ya madini, pia namna ya uwezeshaji wa maono ya Afrika katika sekta ya madini kwa hapa nchini.”

Kwa mujibu wa taasisi hiyo, mjadala utajikita katika kuangalia namna gani sera na kanuni za sekta hiyo nchini vina uhusiano na maono hayo, ambapo pia watatoa mapendekezo ya mwelekeo wa Taifa kuandaa maono katika sekta hiyo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz