MKUU wa mkoa wa Geita, Martin Shigella amesema kuwa mataifa saba yamethibitisha kushiriki Maonesho ya Sita ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mjini Geita. - Shigela amesema hayo leo wakati akizungumuza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bombambili mjini Geita yanapofanyika maonesho hayo yaliyoanza Septemba 20 mwaka huu. - Ametaja mataifa yaliyothibitisha kutoa taasisi na kampuni shiriki kwenye maonesho ni Kenya, Malawi, Burundi, China, India, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wenyeji Tanzania. -
MKUU wa mkoa wa Geita, Martin Shigella amesema kuwa mataifa saba yamethibitisha kushiriki Maonesho ya Sita ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mjini Geita. - Shigela amesema hayo leo wakati akizungumuza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bombambili mjini Geita yanapofanyika maonesho hayo yaliyoanza Septemba 20 mwaka huu. - Ametaja mataifa yaliyothibitisha kutoa taasisi na kampuni shiriki kwenye maonesho ni Kenya, Malawi, Burundi, China, India, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wenyeji Tanzania. - “Tayari washiriki kutoka Burundi wameshawasili, wanaanza kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo, ni wachimbaji wadogo wameungana na serikali ya Burundi kuja kufanya matembezi hayo. - “Wanakuja kushiriki maonesho haya ili wajifunze mambo mapya ya teknolojia, lakini na wenyewe wajifunze namna ya kuratibu maonesho, na hivo kuwezesha nchi zao pia kuandaa maonesho,” amesema. - Amesema hadi sasa takribani washiriki 400 wamethibitisha kushiriki maonesho ya madini kwa mwaka huu ikiwa ni hatua kubwa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikua na washiriki takribani 250. -