Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi 27 kukutana Arusha kujadili utunzaji mbegu, vinasaba

Mbegu Papaiii Nchi 27 kukutana Arusha kujadili utunzaji mbegu, vinasaba

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalam wa kilimo kutoka nchi 27 duniani wanakutana mkoani Arusha katika mafunzo maalum ya kuongeza umahiri na ujuzi wa utunzaji wa mbegu na vinasaba vyake hasa katika vyakula na mboga za Kiafrika.

Wadau hao watajadiliana kuhusu mbinu watakazotumia katika ukusanyaji, uchakataji na utunzaji wa mbegu za mbogamboga ili kuhakikisha usalama wa chakula unaongezeka.

Akizungumza na wadau hao jijini Arusha, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable Center, Dk Gabriel Rugalema alisema ni muhimu mbegu na vinasaba kutunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Amesema nchi 27 ikiwemo za Afrika na Ulaya zinajadiliana kwani suala la mbegu na vinasaba vyake ni suala linalotakiwa kupewa uzito na kuwa kati ya kila nchi tatu za Afrika moja ndiyo yenye benki za mbegu bora hivyo ni vema kutunza mbegu na kuwa eneo hilo ni muhimu kuwekezwa.

"Tunapojenga nyumba, barabara na miundombinu mingine tunaondoa ile ardhi ambayo tungepanda mazao hivyo lazima tuyakusanye haya mazao tuyatunze mahali ili vizazi vijavyo viweze kuyakuta na kuboresha mazao mengine tunayotumia kwa chakula," amesema Dk Rugalema

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya uzalishaji mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Beatrice Banzi amesema ipo haja ya kuwa na mifumo imara na ya kisasa itakayowezesha kutunza mbegu na vinasaba vyake kwani maeneo mengi ya kilimo yamekuwa yakibadilishwa matumizi kwa ajili ya makazi na miundimbinu mingine.

"Ni muhimu kuzingatia utunzaji wa mbegu kwani kuna sababu nyingi zinachangia upotevu wa mbegu kama tunavyoona sasa hivi kuna masuala ya mabadiliko ya tabia nchi," amesema

Kaimu Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari), Emanuel Laswai amesema utunzwaji wa mbegu na vinasaba ukizingatiwa utaongeza usalama na uhakika wa chakula katika nchi za Bara la Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live