Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) umepiga marufuku Raia wa Nchi 20 za Afrika kuingia Dubai huku chanzo kikidaiwa kuwa wengi wao wamekua wakivunja sheria kwa kupitiliza muda waliopangiwa kukaa na kutafuta kazi bila vibali (japo Mamlaka haijathibitisha sababu hizi kwenye taarifa yake).
Mitandao mbalimbali ya Dubai na Afrika imeripoti kuwa Tangazo hilo linasema UAE haitapokea maombi ya visa za siku 30 kutoka kwa Raia wa Uganda, Ghana, Sierra Leone, Sudan, Cameroon, Nigeria, Liberia, Burundi, Jamhuri ya Guinea.
Nchi nyingine ni Gambia, Togo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Senegal, Benin, Ivory Coast, Congo Brazaville, Rwanda, Burkina Faso, Guinea Bissau, Comoro na Jamhuri ya Dominika.