Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nauli meli ya MV Victoria zapaa

Meli One Twioooo Mv Victoria.png Meli ya MV Victoria

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gharama za nauli ya kusafiri kwa njia ya maji kati ya miji ya Mwanza na Bukoba kwa meli ya Mv Victoria "Hapa Kazi Tu" imepanda kwa wastani wa Sh2, 445 hadi Sh10, 000 kwa safari.

Kwa mujibu wa tangazo kwa umma iliyotelewa leo Julai Mosi, 2022 na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) inayosimamia meli za Serikali, bei mpya zitaanza kutumika kuanzia Juali 4.

Tangazo hilo lililotolewa na Idara ya Masoko na Biashara MSCL inaonyesha kuwabnauli za daraja uchumi iliyokuwa Sh16, 000 kwa mtu mzima imepanda hadi Sh21, 000 huku nauli ya watoto ikipanda kutoka Sh8, 550 hadi Sh11, 000.

Abiria watu wazima wanaosafiri katika daraja la biashara ambao awali walilipa nauli ya Sh30, 000 sasa watalipa Sh40, 000 ikiwa ni ongezeko la Sh10, 000 kwa safari.

Wazazi watakaosafiri na watoto wao katika daraja hilo sasa watawalipia nauli ya Sh21, 000 badala ya Sh15, 550 ya awali, ikiwa ni ongezeko la Sh5, 450 kwa safari.

Nauli za daraja la kwanza iliyokuwa Sh45, 000 kwa safari imeongezeka kwa Sh10, 000 hadi kufikia  Sh55, 000 huku watoto ambao awali walilipiwa Sh23, 050 sasa watalipiwa Sh26, 000 watoto, ikiwa ni ongezeko la Sh2, 950 kwa safari.

Advertisement "Nauli mpya zitaanza kutumika rasmi tarehe 4 Julai, 2022" inasema tangazo hilo la kurasa iliyotolewa na MSCL

Akizungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu siyo msemaji wa suala hilo, ofisa mmoja wa MSCL yenye Makao makuu ya jijini Mwanza amethibitisha ongezeko la nauli.

"Mtafute Meneja wa Idara ya Masoko na Biashara kwa maelezo ya kina; lakini kifupi bei mpya hailengi faida kwa sababu MSCL ni kampuni ya umma inayotoa huduma kwa wananchi ambao ndio walipa kodi, bei hizi zinalenga kuiwezesha shirika kumudu gharama za kujiendesha," amesema ofisa huyo

Juhudi za kumtafuta Meneja Idara ya Masoko na Biashara wa MSCL, Anselm Namala kwa ufafanuzi zaidi zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live