Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nanenane kuwapa wakulima mbinu za kilimo, uhifadhi mazao

Nane Nane.jpeg Nanenane kuwapa wakulima mbinu za kilimo, uhifadhi mazao

Sun, 31 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku amewataka wananchi kutumia maonyesho ya wakulima ya Nanenane kupata mbinu za kilimo na uhifadhi wa mazao ili kuepuka janga la njaa.

Maonyesho hayo ya wakulima Kanda ya Mashariki yanayoshirikisha mikoa ya Tanga, Pwani Dar es Salaam na Morogoro, yanatarajiwa kuanza rasmi Agosti Mosi mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Nanenane Manispaa ya Morogoro.

Mwamsiku amesema hayo leo Jumapili Julai 31, 2022 wakati alipotembelea bustani zilizopanda mazao mbalimbali katika viwanja hivyo.

"Kupitia maonyesho haya wakulima na wananchi mbalinbali wanaweza kupata mbinu zitakazowasaidia katika kuhifadhi mazao yao hata baada ya msimu ili kuepuka janga la njaa," amasema.

Mwenyekiti huyo amesema maonyesho ni muhimu kwa Taifa, ikizingatiwa Serikali imejikita katika uchumi wa viwanda na kwamba ili kufanikisha hilo hakuna budi kuhimiza bidhaa za kilimo za kisasa.

"Uchumi wa viwanda ni lazima uende sambamba na kilimo bora chenye mazao yenye tija," amesema.

Zaidi ya watu 500 wakiwamo wakulima na wafugaji wanatarajiwa kushiriki maonyesho hayo yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mjini Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.

Akizungumzia maonyesho hayo meneja wa maandalizi hayo, Venance Segere amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu Agenda 10/30 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi hadi sasa tayari maandalizi yote yamefikia asilimia 80.

"Kila ifikapo Agosti Mosi hadi Nane ya kila mwaka wakulima, wafugaji na wavuvi nchini hutumia siku hiyo kujitokeza katika maonesho maarufu kama Nanenane yaliyoandaliwa mahususi kwa lengo la kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo na mifugo ili kuongeza tija katika shughuli zao,"alisema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz