Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nanai: Watanzania kujadili kilimo leo

59232 NANAIPIC

Thu, 23 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai amewakaribisha Watanzania kushiriki mjadala wa Jukwaa la Fikra utakaojikita kwenye sekta ya kilimo.

Amesema washiriki 500 wanatarajiwa kuujaza ukumbi wa Kisenga uliopo jengo la LAPF jijini hapa, “Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga atakuwapo. Ataambatana na kamishna wa sera na mipango wa wizara hiyo. Watakuwapo watu wa benki na taasisi za fedha pamoja na taasisi za kilimo za ndani na kimataifa. Ni mjadala wenye sura pana,” alisema Nanai.

Kuanzia Juni mwaka jana ilipoanza kuratibu jukwaa hilo, MCL imefanikisha mjadala wa magonjwa yasiyoambukiza kisha ikaangazia maendeleo ya viwanda halafu matumizi ya mkaa.

Alisema leo, masuala mtambuka kuhusu kilimo yatajadiliwa kwa kuangalia fursa zilizopo na kupendekeza suluhu endelevu kwa changamoto wanazokabiliana nazo wakulima.

Kupata suluhu endelevu, Nanai alisema mchango wa kila mmoja unahitajika na akabainisha ndio maana taasisi za kilimo, benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (Sagcot), watafiti na wakulima wenyewe watashiriki.

Chanzo: mwananchi.co.tz